Kings Luxury
Taarifa za kisheria

Sera ya faragha.

Jinsi Kings Luxury inavyokusanya, kuhifadhi, kutumia na kushiriki taarifa binafsi zinazotolewa kupitia tovuti hii.

Utangulizi

Sera hii ya Faragha inazingatia vigezo na masharti ya Kings Luxury. Maana zote zilizofafanuliwa kwenye vigezo na masharti hayo zinatumika pia katika Sera hii ya Faragha.

Faragha yako kama mgeni wa tovuti yetu ni muhimu kwetu. Kwa kuendelea kutumia tovuti hii, unakubali masharti yaliyowekwa katika Sera hii ya Faragha. Unapowasilisha taarifa kupitia tovuti hii, unaridhia ukusanyaji, upangaji, uchakataji na uhifadhi wa taarifa hizo, pamoja na matumizi na utoaji wake kwa mujibu wa sera hii. Tunashauri usome sera hii pamoja na vigezo na masharti yetu kabla ya kuwasilisha taarifa.

Sera hii ya Faragha inaweza kurekebishwa mara kwa mara. Marekebisho yoyote yatawekwa kwenye tovuti hii.

Taarifa zinazokusanywa

Tunakusanya na kuhifadhi taarifa binafsi zinazohitajika kwa maslahi halali ya biashara yetu na makundi ya taarifa binafsi yaliyotajwa katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023). Taarifa hizo zinaweza kujumuisha jina, namba ya simu na jinsia ya mtumiaji, pamoja na taarifa zinazotolewa moja kwa moja, kama vile vidakuzi (cookies) na kumbukumbu za seva. Taarifa hizi zinaweza kuhusisha matumizi na urambazaji wa tovuti, anwani ya IP, muda anaotumia mtumiaji kwenye tovuti na mara anazotembelea tovuti.

Vidakuzi ni taarifa ambazo tovuti huhamisha kwenye hifadhi ya kompyuta ya mtumiaji kwa ajili ya kuweka kumbukumbu. Vidakuzi havidhuru kompyuta yako wala kubeba virusi.

Matumizi ya taarifa

Taarifa binafsi zinazokusanywa kwenye tovuti hii zinaweza kutumika kutoa na kuboresha huduma kwako, pamoja na kuendesha na kuboresha urambazaji na matumizi ya tovuti. Tunaweza pia kutumia taarifa hizi kukutumia taarifa za masoko na matangazo.

Taarifa binafsi zinazokusanywa kutoka kwako zitahifadhiwa na kuchakatwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa binafsi hazitafanyiwa biashara, kuuzwa au kukodishwa kwa wahusika wengine. Ingawa tutajitahidi kutotoa taarifa zako binafsi kwa wahusika wengine bila ridhaa yako au bila sababu zinazohusu maslahi halali ya biashara yetu, hatuhakikishi kwamba taarifa hizo hazitashirikiwa na wahusika wengine bila ridhaa yako.

Unakubali kwamba taarifa zako binafsi zinaweza kushirikiwa na wahusika wafuatao au katika hali zifuatazo, miongoni mwa nyingine:

  • Taasisi za serikali na vyombo vya utekelezaji wa sheria.
  • Watoa huduma za kadi za mkopo na kadi nyingine za malipo.
  • Mhusika ambaye sheria inatutaka tumpe taarifa zako binafsi.
  • Tunapokuwa na sababu ya kuamini kwamba kutoa taarifa ni muhimu ili kumtambua, kuwasiliana naye au kumchukulia hatua za kisheria mhusika anayeweza kuwa anakiuka vigezo na masharti, au anayesababisha madhara au kuingilia, kwa makusudi au bila kukusudia, haki au mali yetu, watumiaji wengine au mtu mwingine yeyote anayeweza kuathiriwa na vitendo hivyo.